Back

UKOMBOZI WA FIKRA -DENIS MPAGAZE

Sh5,000.00

Mara baada ya kupata Uhuru wa Bendera, Mwl. Julius Nyerere alielekeza nguvu katika Uhuru wa Fikra maana aliamini bila Ukombozi wa Fikra, watanzania wataendelea kuishi utumwani. Kwahiyo akapeleka vijana wengi karibu kila kona ya dunia kuutafuta Ukombozi wa Fikra kupitia elimu. Lakini kwa bahati mbaya wengi wakaenda kupambana na mitihani badala ya ujinga. Wakarudi na fikra hatarishi kwa rasilimali za nchi. Mpaka mwalimu anaondoka duniani watanzania bado unamwayamwaya katika Uhuru wa Bendera. Mwalimu katuachia uhuru ambao mwenye nacho ndio binadamu na asiyenacho ni takataka. Uhuru wa wachache kuishi kama malaika na wengi kuishi kama mashetani. Uhuru unaowagawa watu kwa kipato na elimu. Uhuru wa bendera ni sawa na kuvaa suruali isiyo na zipu harusini. Uhuru wa bendera umetujengea nidhamu ya woga kwa manufaa ya wachache kutunyonya kutokana na uoga wetu. Tunahitaji uhuru kamili. Ule uhuru unaoanzia kichwani, yaani uhuru wa fikra. Uhuru utakaotusaidia kuyaona mambo katika uhalisia wake.

-
+
Categories: ,

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “UKOMBOZI WA FIKRA -DENIS MPAGAZE”

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!