Back

MAISHA NI KUTAFUTA SIYO KUTAFUTANA -DENIS MPAGAZE

TZS5,000.00

Mtegemea vya nduguye hufa maskini na vya kupewa hulemaza akili ni methali zinazotukumbusha kwamba utegeaji katika maisha haufai; ni sawa na kupumua kwa kutumia pua ya mwenzako. Hakiwezekani. Kufanya hivyo ni sawa na kusubiri viatu vya marehemu. Utatembea peku hadi miguu iote tende. Maisha yamebadilika sana. Unatakiwa ujue hilo. Tunaishi katika nyakati za ukizubaa unalala njaa hata kama kaka zako wana pesa! Habari za kabla bro hajaoa alikuwa mtu freshi, utazisikia kwa watu wajinga. Kusubili kulishwa ni sawa na kucheza Makirikiri wakati linapigwa Sebene!

-
+
Categories: ,

Jamii yetu imewachoka wasomi. Inawasema vibaya! Wasomi hawaheshimiki tena kama zamani. Eti wasomi wa siku hizihamna kitu. Yaani ni Tabula rasa. Ajabu sana. Mtu ametumia takribani nusu ya maisha yake hapa duniani akisoma anakuja kuitwa hamna kitu. Unajua Mungu anawaona? Kijana mmoja anawatukana walimu kwamba wanazalisha wasomi vihiyo. Acha atukane tu maana mdomo ni mali yake. Anayemtukana mwalimu ni dhahiri hajitambui, maana angejitambua, basi angefahamu kwa nini ualimu ni wito. Sharti la kuwa mwalimu ni kujikana mwenyewe na kuubeba msalaba wa wajinga kwa malipo ya kufedheheshwa. Ndiyo! Mwanafunzi akifeli ni uzembe wa mwalimu, akifaulu ni juhudi zake mwenyewe! Na huu ndiyo wito wenyewe. Asiyekuwa nao hawezi kuitika.

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “MAISHA NI KUTAFUTA SIYO KUTAFUTANA -DENIS MPAGAZE”

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!