Kozi mpya ya Nidhamu, Elimu ya Fedha, Biashara, na Uwekezaji imeandaliwa mahsusi kwa wale wenye shauku ya kuimarisha biashara zao au wanaotafuta njia za kuanzisha vyanzo vipya vya mapato ili kuongeza ustawi wa maisha. Ikiwa unataka kupata maarifa yatakayokusaidia kufanikisha malengo yako ya kifedha na kibiashara, basi uko mahali sahihi!
Kozi hii inaongozwa na wataalamu waliobobea:
- Misana Manyama – Mfanyabiashara mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 15 katika sekta mbalimbali za biashara. Atakufundisha mikakati thabiti ya kuanzisha na kukuza biashara yako.
- Festo Amos – Mwandishi na mkufunzi wa Nidhamu ya Pesa, amechapisha vitabu kama Nguvu ya Pesa, Mikopo na Madeni, na Nidhamu ya Fedha. Ataelekeza mbinu bora za usimamizi wa fedha, kulinda rasilimali zako, na kukusaidia kuepuka mtego wa madeni.
- Victor Mwambene – Mwandishi wa vitabu maarufu kama Kanuni 20 za Fedha na Nguvu ya Kujua, atakufundisha elimu ya fedha, jinsi ya kuanzisha biashara yenye mafanikio, na kukuza biashara yako kwa kutumia maarifa ya kisasa.
Kupitia kozi hii, utajifunza:
- Misingi ya Usimamizi wa Fedha – Jinsi ya kutunza na kuongeza kipato chako kwa nidhamu thabiti ya kifedha.
- Mikakati ya Biashara – Namna ya kubuni na kutekeleza mipango bora ya kibiashara inayokuza faida na ustawi wa biashara.
- Uwekezaji – Fursa mbalimbali za uwekezaji na jinsi ya kufanya maamuzi yenye tija kwa ajili ya muda mrefu.
- Stori za Mafanikio – Utaelezwa hadithi za kweli za wajasiriamali waliofanikiwa, pamoja na changamoto walizopitia, ili kujifunza kutoka kwa uzoefu wao wa maisha.
Iwe unaanzisha biashara mpya au unataka kuikuza biashara uliyonayo, kozi hii itakupa nyenzo muhimu za kukusaidia kufikia mafanikio. Jifunze pamoja nasi na uanze safari yako ya kifedha kwa mafanikio! Karibu tujifunze pamoja!
Course Features
- Lectures 7
- Quiz 0
- Duration Lifetime access
- Skill level All levels
- Language Swahili
- Students 698
- Certificate No
- Assessments Self