Mwaka 2018 nilitafutwa na kampuni moja kubwa ambayo ilikuwa inatoa mitaji kwa kampuni zingine 8 zilizoko bara na visiwani kwa ajili ya kuwasaidia kufanikiwa zaidi katika biashara zao.
Katika historia ya kampuni hizi, zilikuwapo zingine ambazo walishawahi kuongezewa mitaji mara kadhaa lakini hazikupata mabadiliko yoyote yale na kuna zingine ambazo zilikuwa zinajitangaza sana ila hawakuona mabadiliko yoyote.
Kuna baadhi ya kampuni hizi zilikuwa tayari zimeanza kupata shida ya kulipa wafanyakazi wao na wengine walikuwa wanakabiliwa na madeni makubwa sana ya kibiashara ambayo ilikuwa inaonekana wazi kabisa kuwa haitawezekana
kuyalipa.
Jukumu langu la kwanza nililopewa ni kufanya mabadiliko yatakayochukua mwaka mmoja ili kuwasaidia kuanza kuinuka tena kibiashara. Baada ya kuyafanyia uchambuzi na kutengeneza mbinu za kubadilisha namna wanavyoendesha mambo yao, nilianza kufanya nao program mara moja. Ilipofika miezi mitatu, kampuni zote zilizokuwa kwenye program zilianza kuongeza mauzo yao na aliyepata chini kabisa ilikuwa ni wale ambao walipata ongezeko la mauzo kwa 35%.
Ingawa ilikuwa inaonekana kuwa kampuni hizi zilikuwa zinaelekea kufa, hakuna hata moja ambayo ilikufa na yote yanaendelea vizuri kwa sasa na yameendelea kufanikiwa kimauzo na kuongeza thamani ya mitaji yao.
Siri hizi walizozitumia kuleta mabadiliko katika biashara zao, unaweza kuzitumia pia kuleta mabadiliko katika baishara yako pia. Bila kujali hali ya biashara yako ya sasa, mbinu hizi ambazo niliendelea kuzifundisha kwa wafanyabiashara mbalimbali kuanzia wa chini, wa kati na wa juu, zimewaletea matokeo makubwa sana.
Course Features
- Lectures 12
- Quiz 0
- Duration Lifetime access
- Skill level All levels
- Language Swahili
- Students 448
- Certificate No
- Assessments Yes